09-09-2023

Viongozi wakuu wa CBCA wazungumuza na Wachungaji Wastaafu wa Poste Katwa pa Butembo CBCA Kalimbute

Leo, Jumamosi tarehe 9 Septemba 2023, Prezidenti na Kiongozi mkuu wa CBCA, Mchungaji Dkt. Jonathan Kivatsi, alikutana na wachungaji wastaafu wa Posta Katwa hapa Butembo. Mkutano huo ulifanyika katika Usharika wa CBCA Kalimbute, ambapo pia alishiriki katika ibada ya asubuhi kama Mhubiri. Mkutano huo ni sehemu ya ziara yake ya kazi katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini, ambapo alifika tangu siku ya tatu kwa kuufanya Mkutano mkuu wa CBCA wa mara ya 44 pa Kikyo. 

Katika mkutano huo leo, Mchungaji Dkt. Jonathan Kivatsi aliwashukuru wachungaji wastaafu kwa huduma waliyotoa kwa Mungu ndani ya Kanisa la Bwana, na pia aliwahimiza kuendelea kuomba kwa ajili ya kanisa, CBCA. Alisema kuwa wachungaji wastaafu ni hazina kubwa kwa kanisa, kwani wana uzoefu, hekima na ushuhuda wa kuigwa na vizazi vijavyo. Aliongeza kuwa CBCA inathamini mchango wao katika ujenzi wa ufalme wa Mungu na inawajali mahitaji yao.

Mwisho wa mkutano huo, namba 1 ya CBCA aliwapa ng’ombe kama ishara ya kutambua kazi zao, kumaanisha shukrani za CBCA kwa wachungaji wastaafu. Wao pia walimpa mbuzi nene kwa ajili ya mageuzi mbalimbali ndani ya Kanisa leo kumaanisha baraka za Mungu kwa Prezidenti na Kiongozi mkuu wa CBCA. Walimwombea yeye na timu yake yote ya uongozi wa CBCA, wakiomba Mungu awape hekima, nguvu na neema katika utumishi wao. Mkutano huo ulimalizika kwa furaha na shangwe, huku wachungaji wastaafu wakimshukuru Mchungaji Dkt. Jonathan Kivatsi kwa kuwatembelea na kuwakumbuka.

 

Huduma ya Mawasiliano CBCA

0 commentaire(s)

Aucun commentaire pour l'instant...

Laissez un commentaire